Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Jacob Mkunda (kulia) akimvisha nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu.
Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena akikata utepe kuzindua boti ya uvuvi ya MV Bulombora inayotarajiwa kufanya shughuli zake kwenye ziwa Tanganyika inayomilikiwa na Kikosi cha JKT Bulombora mkoani Kigoma.
Vijana wa JKT Operesheni Miaka 60 ya jeshi hilo kujitolea, wakiwa katika gwaride la kuhitimisha mafunzo yao ya awali ya kijeshi katika Kikosi cha JKT Mlale, mkoani Ruvuma.
Shughuli za kilimo ndani ya JKT hususani zao la chikichi kupitia Kikosi chake cha Bulombora mkoani Kigoma hutekelezwa kwa kushirikiana na vijana wanaopatiwa mafunzo ya JKT kama inavyoonekana katika picha hii.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon akimlisha mnyama aina ya twiga wanaopatika kwenye bustani ya wanyama pori (Zoo) ya Ruvu JKT Wildlife katika mkoa wa Pwani baada ya kuzinduliwa na kuanza kutoa huduma za utalii.
Baadhi ya wanyama pori aina pundamilia na pofu wanaopatikana katika bustani (zoo) ya Ruvu JKT Wildlife inayopatikana mkoa wa Pwani iliyopo karibu na eneo la burudani la Ruvu JKT Club, barabara ya Morogoro.
Moja ya vyombo vilivyoundwa na Serikali ya Tanganyika mara tu baada ya Taifa hili kupata uhuru ni Jeshi la Kujenga Taifa lililoasisiwa tarehe 10 Jul 1... Soma zaidi
Dira
Kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa, hatimaye Tanzania iwe ni jamii yenye nidhamu, umoja, uzalendo , undugu, ukakamavu na kupenda kazi.
Dhima
Kuwalea vijana wa Tanzania, ili kuwajengea nidhamu, uzalendo, ukakamavu na kuwafundisha ujuzi hatimaye kuchangia katika ulinzi wa Taifa na maendeleo ya kiuchumi