Tanzania emblem
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

JESHI LA KUJENGA TAIFA -JKT

Washiriki wa Kozi ya NDC Watembelea JKT

14 Mar, 2025
Washiriki wa Kozi ya NDC Watembelea JKT

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema ziara za Washiriki wa Kozi ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC) wanazofanya Makao Makuu ya JKT kila mwaka, zimekuwa chachu ya mafanikio kwa Jeshi hilo hasa katika nyanja za Stratejia ya Ulinzi katika Taifa hili. 

Meja Jenerali Mabele amesema hayo hivi karibuni Makao Makuu ya JKT Chamwino Dodoma, wakati wa ziara ya kimafunzo ya Washiriki wa Kozi ya Kundi la 13, 2024/25, kutoka chuo cha NDC Kunduchi, jijini Dar es Salaam.

Aidha, Meja Jenerali Mabele amesisitiza kuwa JKT linapata faida zaidi kutokana na ziara ya Washiriki hao, “Tunapata nafasi ya wao kutushauri namna ya kuendesha Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa ubora zaidi, kwa hiyo sisi kwetu kozi hii kuja kututembelea hapa kwetu tunafurahi, Kila wanapokuja wanatupa mawazo ya kuboresha Mafunzo ya JKT” amesema Meja Jenerali Mabele.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), Balozi Meja Jenerali Wilbert Ibuge amelishukuru JKT kwa mapokezi na kukubali uwezeshaji wa dhumuni lao ziara hiyo iliyolenga kuwajengea uwezo Washiriki wa Kozi wa kutunga sera na utekelezaji wake, kuwashauri viongozi wa juu Serikalini na Taasisi zake ili kufanya maamuzi yenye maslahi ya Taifa na kuendeleza uhusiano katika Jumuiya za Kimataifa.

Kozi hiyo imejumisha Washiriki kutoka nchi 16 ikiwemo Kenya, Zambia, Uganda, Malawi, Nigeria, Afrika ya Kusini, Misri, India, Zimbabwe na Bangladesh, Mataifa mengine ni Botswana, Namibia, Burundi, Sierra Leone, Ethiopia, Rwanda na wenyeji Tanzania.