Tanzania emblem
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

JESHI LA KUJENGA TAIFA -JKT

Mafanikio ya jumla JKT

Kwa ujumla JKT limefanikiwa katika sekta mbali mbali kama ifuatavyo:

1. JKT limesaidia kuimarisha umoja wa Kitaifa. Vijana wengi waliopitia JKT wameonesha moyo wa kupenda kazi za mikono, kujituma na kujiheshimu.

2. Miongoni mwa vijana waliopitia JKT wameonesha kuwa viongozi mahiri, wachapa kazi, wenye nidhamu, wabunifu na wavumilivu.

3. Vijana wa JKT wamechangia kwa kiasi kikubwa katika kuthamini na kuhifadhi utamaduni wa Taifa.

4. JKT limetoa wanamichezo bora, wenye viwango vya kitaifa na kimataifa na hivyo kuiletea sifa nchi yetu.

5. JKT limewaandaa vijana kuwa tayari kuitumikia nchi katika majanga kama mafuriko, moto na ajali nyinginezo

6. JKT ni taasisi inayotoa mafunzo ya stadi za kazi na stadi za maisha, vijana waliopitia JKT wanaendesha maisha yao kwa kutumia ujuzi na uzoefu walioupata JKT.

7. JKT limekuwa mfano wa kuigwa na mataifa jirani na hivyo kuwa chachu kwa mataifa hayo kuanzisha shughuli za malezi ya vijana katika nchi zao. Mataifa ya Zambia, Msumbiji na mengine yamejifunza kutoka Tanzania.

8. Uhifadhi wa mazingira umepewa umuhimu mkubwa. Taasisi na wananchi wanaoishi jirani na vikosi vya JKT, hupewa miche ya miti bure au huuziwa kwa bei ya chini ili kuwawezesha kutunza na kuhifadhi mazingira.