under construction

UJUE UTARATIBU WA KUJIUNGA NA JKT

JKT huandikisha vijana wa kujitolea kutoka mikoa yote ya hapa nchini kila mwaka. Utaratibu unaotumika ni kwa JKT kuandika barua kwa wakuu wa Mikoa na kuanisha nafasi ambazo mkoa umetengewa.

Baada ya Mkoa kupata barua kutoka kwa Mkuu wa JKT na idadi ya nafasi za vijana waliopangiwa kujiunga. Mkoa hugawa nafasi hizo kulingana na wilaya zake. Pia wilaya zinatakiwa kupeleka katika tarafa, kata na vijiji. Mara nyingi uongozi wa wilaya hubandika tangazo la nafasi hizo katika ubao wao wa matangazo. JKT hutangaza nafasi za kujiunga na jeshi hilo kupitia vyombo vya habari vya Serikali na biafsi kwa nia ya kuharakisha taarifa kuwa. kia wananchi hasa vijana. Usaili wa awali hufanyika chini ya Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya wanakotoka vijana hao, baadaye hufanyika mkoani, ili kupata idadi ya vijana wa mkoa mzima.

Zoezi hilo linapokamilika mikoani, JKT hutuma timu za maafisa na askari kutoka Makao Makuu ya JKT kwa ajili ya kuhakiki vijana waliosailiwa katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Vijana hupimwa afya zao na kusafirishwa katika vikosi vya JKT.

Kabla ya kuondoka timu za usaili kutoka JKT hufanyiwa semina na kuelekezwa jinsi ya kubaini udanganyifu wa vyeti bandia vya kuzaliwa na shule. Mhariri Mkuu wa Jarida la Vijana Leo alikuwa ni miongoni mwa watu walioshiriki usaili mkoani Ruvuma. Vijana wa mkoa huo walitoka katika Wilaya za Songea Mjini, Vijijini, Namtumbo, Mbinga na Tunduru na kukusanyika Makao Makuu ya Mkoa wa Ruvuma. Vijana hao walikuwa na shauku ya kupata nafasi ya kujiunga na JKT.