Jumanne, 17 Mei 2022

Majukumu ya Jeshi la Kujenga Taifa

MAJUKUMU YA MSINGI( Objectives)

1. Malezi ya Vijana

 • Vijana kufundishwa moyo wa kupendana bila kujali tofauti za itikadi, dini, kabila na kipato.
 • Kupenda kazi za mikono.
 • Kuthamini na kuendeleza mila, desturi na kudumisha utamaduni wa Taifa.
 • Kuwa raia wema, wanaojiamini, wanaojituma, wenye uzalendo na kuipenda nchi yao.

2.Ulinzi wa Taifa

 • Kuwapa vijana mbinu za kijeshi wawe Jeshi la akiba, kuwaandaa vijana watakaofaa kujiunga na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.
 • Kuwaandaa vijana kusaidia katika majanga mbalimbali, mfano mafuriko, moto na ajali mbali mbali.

3.Uzalishaji Mali

  Ili kuwafanya vijana wa kitanzania waepukane na kusumba kuwa kazi za ofisini ndio njia pekee na bora inayomuwezesha mtu kuishi, JKT linahusika na uzalishaji mali kwa lengo la kuwawezesha vijana kujiajiri katika sekta mbali mbali mara baada ya kumaliza mkataba na JKT. Uzalishaji mali unaofanywa na JKT ni pamoja na:-
 • Kujenga na kukarabati majengo
 • Viwanda na Kilimo
 • Madini na Nishati
 • Utalii
 • Ulinzi kwa Taasisi binafsi (Security Guard Services)
 • Maduka (Super Market)
 • Kuunganisha magari na mitambo
 • Huduma za elimu

Uadilifu

JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa

Umoja na Mshikamano

Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.

Kujitolea

Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.

Uzalendo

Huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.

Nidhamu

Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.

Kupenda kazi

Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi