MAADILI YA MSINGI (Core values)
JKT linaendeshwa kwa kufuata misingi na maadili ya kujenga umoja na mshikamano wa Kitaifa. Maadili ya msingi ya JKT ni yafuatayo:-
Uadilifu
- JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa.
Kujitolea
- Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.
Umoja na Mshikamano
- Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.
Uzalendo
- huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.
Nidhamu
- Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.
Kupenda kazi
- Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi.