Jumanne, 17 Mei 2022

Kuhusu Jeshi la Kujenga Taifa

Moja ya vyombo vilivyoundwa na Serikali ya Tanganyika mara tu baada ya Taifa hili kupata uhuru ni Jeshi la Kujenga Taifa lililoasisiwa tarehe 10 Jul 1963. Jeshi la Kujenga Taifa au kwa kifupi JKT, liliundwa ili kuponya majeraha yaliyoachwa na serikali ya kikoloni miongoni mwa jamii ya watanzania ambayo ni pamoja na ubaguzi miongoni mwao katika misingi ya kidini, makabila, rangi na kipato. Chombo hiki ni muhimu katika kuelimisha na kuandaa vijana wa kitanzania kiuzalendo, kimaadili, kinidhamu na kuwafanya raia wema wanaopenda kutumikia na kulinda nchi yao.

Vikosi vya JKT ni mahali ambapo vijana hupata fursa ya kujifunza kikamilifu na kwa vitendo, maana na umuhimu wa kazi na pia kujifunza kutoa huduma kwa Taifa lao bila kutegemea kulipwa ujira wowote. Kwa hiyo, imedhihirika wazi ya kuwa wajibu wa JKT katika maendeleo ya Taifa hili ni mkubwa na muhimu sana.

Nchi mbalimbali duniani zina taasisi zinazofanana na taasisi yetu ya JKT. Kwa msingi huo nchi yetu kuwa na JKT ni jambo la kujivunia sana. JKT vilevile ni chombo cha kujenga Umoja na Utaifa kwa vijana wetu.

DIRA  (Visions)

  Kupitia JKT, Tanzania iwe ni nchi ambayo vijana wake watalelewa vizuri katika malezi yaliyo bora wakiwa wenye:-
 • Nidhamu
 • Kujiamini
 • Moyo wa uzalendo na kuipenda nchi yao
 • Umoja na Udugu
 • Moyo wa kupenda kazi
 • Kutekeleza wajibu wao.

DHIMA (Missions)

  Kuwalea vijana wa Tanzania ili wawe na nidhamu, uzalendo na ujuzi ambao utawawezesha kushiriki kikamilifu katika Ulinzi, Usalama pamoja na Ujenzi wa Taifa.

MAJUKUMU YA MSINGI( Objectives)

1. Malezi ya Vijana

 • Vijana kufundishwa moyo wa kupendana bila kujali tofauti za itikadi, dini, kabila na kipato.
 • Kupenda kazi za mikono.
 • Kuthamini na kuendeleza mila, desturi na kudumisha utamaduni wa Taifa.
 • Kuwa raia wema, wanaojiamini, wanaojituma, wenye uzalendo na kuipenda nchi yao.

2.Ulinzi wa Taifa

 • Kuwapa vijana mbinu za kijeshi wawe Jeshi la akiba, kuwaandaa vijana watakaofaa kujiunga na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.
 • Kuwaandaa vijana kusaidia katika majanga mbalimbali, mfano mafuriko, moto na ajali mbali mbali.

3.Uzalishaji Mali

  Ili kuwafanya vijana wa kitanzania waepukane na kusumba kuwa kazi za ofisini ndio njia pekee na bora inayomuwezesha mtu kuishi, JKT linahusika na uzalishaji mali kwa lengo la kuwawezesha vijana kujiajiri katika sekta mbali mbali mara baada ya kumaliza mkataba na JKT. Uzalishaji mali unaofanywa na JKT ni pamoja na:-
 • Kujenga na kukarabati majengo
 • Viwanda na Kilimo
 • Madini na Nishati
 • Utalii
 • Ulinzi kwa Taasisi binafsi (Security Guard Services)
 • Maduka (Super Market)
 • Kuunganisha magari na mitambo
 • Huduma za elimu

Maadili ya msingi (Core values)

MAADILI YA MSINGI (Core values)

JKT linaendeshwa kwa kufuata misingi na maadili ya kujenga umoja na mshikamano wa Kitaifa. Maadili ya msingi ya JKT ni yafuatayo:-

Uadilifu

  • JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa.

Kujitolea

  • Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.

Umoja na Mshikamano

  • Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.

Uzalendo

  • huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.

Nidhamu

  • Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.

Kupenda kazi

 • Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi.

Uadilifu

JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa

Umoja na Mshikamano

Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.

Kujitolea

Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.

Uzalendo

Huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.

Nidhamu

Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.

Kupenda kazi

Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi