Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Angola Mhe. Joao Dos Santos (kushoto), akijionea bidhaa zinazotengenezwa na Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha SUMAJKT Shoes and Leather Products Co. Ltd kilichopo Mlalakuwa, Jijini Dar es Salaam Wakati wa ziara yake Makao Makuu ya SUMAJKT. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT, Brigedia Jenerali Petro Ngata.
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Salum Haji Othman akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo la Ghorofa moja ambalo limejengwa kwa matumizi ya madarasa ya wanafunzi katika chuo hicho, Wa pili kulia ni Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele.
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa Kozi ya Uongozi Mdogo Kundi la 13, 2024/25 katika Chuo cha Uongozi JKT kilichopo Kimbiji, Kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Kanali Festus Mang’wela.
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Angola Mhe. Joao Dos Santos akiwa katika ziara ya kutembelea kikosi cha Ruvu JKT kilichopo Mlandizi mkoani Pwani, alipata fursa ya kutembelea Bustani ya Wanayama Pori Walio wapole ya Ruvu JKT Wildlife na kumlisha chakula mnyama aina ya twiga.
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele akikagua mojawapo ya gari aina ya Isuzu D Max Pickup muda mfupi baada ya uzinduzi wa magari hayo, Makao Makuu ya JKT, Chamwino.
Magari idadi tisa aina ya Isuzu D Max Pickup yaliyonunuliwa na JKT kwa matumizi ya Kiutawala Makao Makuu ya JKT na Vikosini muda mfupi kabla ya uzinduzi wake yakiwa tayari kutumika.
Moja ya vyombo vilivyoundwa na Serikali ya Tanganyika mara tu baada ya Taifa hili kupata uhuru ni Jeshi la Kujenga Taifa lililoasisiwa tarehe 10 Jul 1... Soma zaidi
Dira
Kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa, hatimaye Tanzania iwe ni jamii yenye nidhamu, umoja, uzalendo , undugu, ukakamavu na kupenda kazi.
Dhima
Kuwalea vijana wa Tanzania, ili kuwajengea nidhamu, uzalendo, ukakamavu na kuwafundisha ujuzi hatimaye kuchangia katika ulinzi wa Taifa na maendeleo ya kiuchumi