Jumanne, 02 Machi 2021

Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe.Dkt Hussein Mwinyi anaendelea na ziara yake Kanda ya Kati. Ametembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya SUMA JKT lililopo Dodoma lenye ghorofa sita ambapo thamani ya mradi huo ukikamilika ni Tshs 1.8 Bilioni.

 

Uadilifu

JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa

Umoja na Mshikamano

Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.

Kujitolea

Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.

Uzalendo

Huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.

Nidhamu

Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.

Kupenda kazi

Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi