Jumanne, 28 Septemba 2021

. Featured

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa ,Maafisa,Askari,Vijana na Watumishi wote wa Umma JKT,wanatoa Pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Samia Suluhu Hassan,Familia na Watanzania wote kwa ujumla, kwa msiba mkubwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na JKT Hayati Mhe.Elias John Kwandikwa"Tunayafanyia kazi yale yote uliotuachia" Pumzika kwa Amani.

 

Uadilifu

JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa

Umoja na Mshikamano

Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.

Kujitolea

Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.

Uzalendo

Huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.

Nidhamu

Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.

Kupenda kazi

Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi