.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Martin Busungu, akitoa salamu za mwisho kwa askari na vijana wa JKT waliofariki kwa ajali mkoani Mbeya.
Ziara ya Mkuu wa JKT-Bulombora
Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Raphael Muhuga, akiwasalimia vijana wa JKT waliopata ajali ya gari iliyotokea Oktoba Mosi mwaka huu majira ya saa 10:30 jioni katika Kijiji cha Kasaka eneo la mzani, wakisafiri kuelekekea mjini Kigoma kikazi, baada ya lori aina ya IVECO namba 5717 JW 09, mali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kambi ya JKT Bulombora, kupasuka magurudumu yake ya nyuma na kupinduka.
Ziara ya Mkuu wa JKT
Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Raphael Muhuga, akiwa katika picha ya pamoja na makamanda wa Kambi ya JKT Bulombora alipofanya ziara kwenye kambi hiyo.
Uzinduzi wa Magari Kampuni ya Ulinzi SUMAGUARD
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) SUMAJKT akizindua mioja ya magari yaliyonunuliwa na Kampuni ya ulinzi SUMAGUARD , Wanao shuhudia tukio hilo ni Mkuregenzi Mtendaji SUMAJKT Kanali Andrew Samillan pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya SUMAGUARD LTD Capt Mwaijande.
Mkuu wa Utawala na Mafunzo Brigedia Jenerali Jacob Kingu akikagua mashamba ya Mahindi
Mkuu wa Utawala na Mafunzo Brigedia Jenerali Jacob Kingu alipokuwa akikagua mashamba ya Mahindi yanayolimwa na vikosi vya JKT alipokuwa ziarani kwenye vikosi vya JKT mkoani Tanga hivi karibuni
Uzinduzi wa Magari Kampuni ya Ulinzi SUMAGUARD LTD
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) SUMAJKT akizindua mioja ya magari yaliyonunuliwa na Kampuni ya ulinzi SUMAGUARD , Wanao shuhudia tukio hilo ni Mkuregenzi Mtendaji SUMAJKT Kanali Andrew Samillan pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya SUMAGUARD LTD Capt Mwaijande.
Mkuu wa Utawala na Mafunzo akikagua Mabweni ya Vijana -Tanga
Mkuu waUtawala na Mafunzo Brigedia Jenerali Jacob Kingu akikagua moja ya mabweni ya kulala vijana wa JKT alipokuwa ziarani katika vikosi vya JKT mkoani Tanga
SUMAGUARD LTD
Gari ambalo limenunuliwa na Kampuni ya Ulinzi ya SUMAGUARD katika kujiimarisha kiutendaji kazi.
Mlalakuwa JKT
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael Muhuga akifurahi jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Andrew Samillan baada ya kukata utepe kuzindua moja ya gari lililonunuliwa na Kampuni ya Ulinzi ya SUMAGUARD LTD tukio lililofanyika Makao Makuu ya JKT Mlalakuwa Dar es Salaam.
Mkuu wa Utawala na Mafunzo ziarani Tanga
Mkuu wa utawala na Mafunzo Brigedia Jenerali Gideon Kingu alipokuwa ziarani mkoani Tanga kukagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na JKT.