Jumapili, 21 Oktoba 2018
20 Okt
.

.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Kanali Mabele akiwa mkoani Morogoro akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa jengo la kisasa la Maabara ya Sayansi ya Chuo ya Chuo Kikuu cha kKilimo cha Sokoine (SUA) unaojengwa na Kampuni ya ujenzi wa SUMA JKT. Mradi huo una thamani ya Tshs 4.7 Bilioni ulianza tarehe 03 Julai 2018 na unatarajiwa kumalizika tarehe 28 Februari 2019. Picha hapo juu.

20 Okt
.

.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Kanali Rajabu Mabele alipotembelea mradi wa ujenzi wa Hosteli za wanachuo wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro unaojengwa na Kampuni ya ujenzi ya SUMA JKT. Mradi huo wa majengo manne ya gorofa tatu yenye uwezo wa kulaza wanachuo 250 kila jengo unathamani ya jumla ya Tshs 6.5 Bilioni na unategemea kukamilika ndani ya kipindi cha miezi 15. Picha hapo juu.

11 Okt
.

.

 

 

Vijana wa Kujitolea Operesheni Magufuli wa Kambi ya Mtabila JKT Mkoani Kigoma wakifanya Mtihani wa mwisho wa Stadi za Kazi na Stadi za Maisha leo tarehe 11 October 2018. Vijana watakaofaulu watapatiwa Vyeti vya kuhitimu Masomo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Mtihani huo wa Masomo nane (8) unaofanywa na Vijana wa Operesheni Magufuli waliopo katika Makambi ya JKT nchini, Wameanza tarehe 09 October 2018 na wanamaliza leo tarehe 11 October 2018. Picha hapo juu. 

11 Okt
.
10 Okt
.

.

 

Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe.Dkt Hussein Mwinyi amehitimisha ziara yake ya kikazi ya kutembelea miradi mbalimbali ya SUMA JKT iliyopo Kanda ya Nyanda za juu Kusini kwa kutembelea Kikosi cha Itende JKT Mkoani Mbeya na Kupatiwa taarifa ya utendaji kazi wa Kikosi pamoja Kanda ya ujenzi ya SUMA JKT. Akiwa Itende JKT amekagua Kiwanda cha kubangua kahawa, Shamba la kahawa lenye ukubwa wa hekari 200 na baadae kuzindua jengo la mlango mkuu. Katika ziara hiyo, Mhe. Waziri anaambatana na Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Martin Busungu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Kanali Rajabu Mabele. Picha hapo juu.

 

 

 

 

 

 

Uadilifu

JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa

Umoja na Mshikamano

Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.

Kujitolea

Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.

Uzalendo

Huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.

Nidhamu

Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.

Kupenda kazi

Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi