Alhamisi, 17 Januari 2019
18 Des
.

.

 

Magari yanayotumika kusambaza Maji ya Uhuru Peak kutoka Kiwanda cha SUMAJKT.

18 Des
.

.

 

Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Martin Busungu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Magari ya kusambaza Maji ya "Uhuru Peak" yanayotengenezwa na kiwanda cha SUMAJKT.

12 Des
.

.

 

Waziri wa Madini, Mhe. Angela Kairuki akipokea maelezo mafupi kutoka kwa Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Martin Busungu

12 Des
.

.

 

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Martin Busungu. akiwa kwenye mkutano wa pamoja na Makamanda wa Vikosi vya JKT, Wakuu wa Shule za Sekondari za JKT na Mameja wa Kanda za Ujenzi za SUMAJKT.

20 Nov
.

.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe.Ahaj.Dkt Hussein Ali Mwinyi akiwa ziarani Mkoani Mtwara. Dkt Mwinyi amefanya ziara hiyo kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama yanayohusu usombaji na uhifadhi wa zao la Korosho. Ziara hii ya Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ni ya kawaida ya kikazi inayolenga kuhakikisha maelekezo ya Amiri Jeshi Mkuu yanatekelezwa kikamilifu na itahusisha mikoa yote inayozalisha zao hilo la korosho. Picha hapo juu. 

Uadilifu

JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa

Umoja na Mshikamano

Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.

Kujitolea

Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.

Uzalendo

Huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.

Nidhamu

Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.

Kupenda kazi

Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi