Jumanne, 17 Mei 2022

 

 

 

 

TAARIFA KWA UMMA

 

WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA KUJITOLEA MWAKA 2020

 

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge, anawatangazia Vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani nafasi za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea kwa mwaka 2020.

 

Utaratibu wa Vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo, unaratibiwa na Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambako mwombaji anaishi.

 

Utaratibu wa maandalizi ya Vijana hao kwaajili ya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea unaanza mwezi Agosti 2020. Vijana watakaoteuliwa wanatakiwa kuripoti kwenye Makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa mwezi Oktoba 2020.

 

Aidha, Jeshi la Kujenga Taifa linapenda kuwataarifu Vijana watakaopata fursa hiyo kuwa halitoi ajira kwa vijana, Pia halihusiki kuwatafutia Vijana ajira katika Asasi, Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Mashirika mbalimbali ya Serikali na yasiyo ya Kiserikali, Bali hutoa mafunzo ambayo yatawasaidia Vijana kujiajiri wenyewe mara baada ya kumaliza Mkataba wao na Jeshi la Kujenga Taifa.

 

 

Sifa za Muombaji ni kama ifuatavyo-:

1.     Awe Raia wa Tanzania

2.     Elimu na Umri

        a.       Vijana wenye elimu ya Darasa la Saba, umri ni kuanzia miaka 16 hadi 18.

        b.       Vijana wenye elimu ya Kidato cha Nne, umri usiwe zaidi ya miaka 20

        c.       Vijana wenye elimu ya Kidato cha Sita umri usiwe chini ya miaka 18 na usiwe zaidi ya miaka 22.

        d.       Vijana wenye elimu ya Stashahada umri usizidi miaka 25.

        f.        Vijana wenye elimu ya Shahada, umri usiwe zaidi ya miaka 26.

        g.       Shahada ya uzamili, umri usiwe zaidi ya miaka 30.

        h.       Vijana wenye elimu ya Shahada ya Uzamivu, umri usizidi miaka 35.

        j.        Vijana waliohitimu elimu ya msingi waje na vyeti halisi

        k.       Kijana Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)

        l.        Kijana Awe na cheti halisi cha kuhitimu elimu ya sekondari (School Leaving Certificate)

       m.       Kijana Awe na cheti cha taaluma (Original Academic Certificate /Transcript)

           n.        Kwa vijana waliomaliza elimu ya sekondari Kidato cha Nne na sita  wawe na ufaulu ufuatao.

                  (i)       Kidato cha nne Wawe na ufaulu wa alama      zisizopungua 32

                  (ii)      Kidato cha sita wawe na ufaulu daraja la kwanza hadi daraja la Nne.

3.     Awe na afya njema, akili timamu na asiwe na alama yoyote ya mchoro mwilini (Tattoo)

4.     Awe mwenye Nidhamu na tabia nzuri na awe hajawahi kupatikana na hatia Mahakamani na hajawahi kufungwa.

5.     Asiwe ametumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au KMKM wala kuajiriwa na idara nyingine Serikalini.

6.     Asiwe amepitia JKT katika operesheni za nyuma.

7.     Asiwe amejihushisha na matumizi ya dawa za kulevya, bangi au yanayofanana na hayo.

8.     Kwa wale wenye vipaji vya michezo mbalimbali na Sanaa, sifa za elimu ni sawa na zilizotajwa hapo juu.

 

JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo:-

1.     Bukta ya rangi ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni (elastic) iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini isiyo na zipu.

2.     Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.

3.     Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.

4.     Soksi ndefu za rangi nyeusi.

5.     Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.

6.     Truck suit ya rangi ya kijani au blue.

7.     Flana ya kijani kibichi yenye kola ya duara isiyo na maandishi.

8.     Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.

 

Aidha, Kutokana na Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID-19) Nchini, Tahadhari za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kama zilivyoelekezwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya zitazingatiwa kwa kipindi chote vijana watakapokuwa makambini.

 

Mkuu wa JKT Meja Jenerali Charles Mbuge anawaalika Vijana wote watakaopata fursa hiyo kuja kujifunza Uzalendo, Ukakamavu, Stadi za Kazi, na Stadi za Maisha na pia kuwa tayari kulilinda na kulitumikia Taifa letu.

 

 

 

 

 

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,

Makao Makuu ya JKT,

Tarehe 20 Agosti 2020.

Uadilifu

JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa

Umoja na Mshikamano

Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.

Kujitolea

Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.

Uzalendo

Huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.

Nidhamu

Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.

Kupenda kazi

Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi