TAARIFA KWA UMMA
WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2021
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenerali Rajabu Mabele anawataka kuripoti Makambini vijana wote walioitwa kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria kwa mwaka 2021 ambao mpaka sasa hawajaripoti.
Aidha, Jeshi la Kujenga Taifa limetoa nyongeza ya majina ya Vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita mwaka 2021 kwenda kuungana na vijana wenzao walioitwa hapo awali kuhudhuria mafunzo hayo.
Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria mwaka 2021 yataendeshwa kwa muda wa miezi mitatu tu, Vijana hao walioitwa katika orodha ya pili na wale ambao hawajaripoti hadi sasa wanatakiwa kuripoti makambi ya JKT waliyopangiwa mara moja, Mwisho wa kuripoti ni tarehe 17 Juni 2021.
Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical disabilities) waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.
Orodha kamili ya nyongeza ya majina ya vijana walioitwa, Makambi ya JKT waliyopangiwa na maeneo yaliyopo pamoja na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo, Inapatikana hapo chini.
BOFYA JINA LA KIKOSI HAPO CHINI KUANGALIA NYONGEZA YA MAJINA YA VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA 2021
Tafadhali bonyeza jina la kikosi kutafuta jina lako
Mkuu wa JKT Brigedia Jenerali Rajabu Mabele, Anawakaribisha vijana wote walioitwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya JKT,
Tarehe 10 Juni 2021.