Jumanne, 24 Novemba 2020

 

 

 

TAARIFA KWA UMMA

 

WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2020

 

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2020, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria.

 

Sanjari na uchaguzi huo, JKT limewapangia makambi watakayo kwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 24 hadi 27 Julai 2020. Aidha, mafunzo hayo yatafunguliwa kuanzia 01 Agosti 2020.

 

Vijana waliochaguliwa wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma - Mara, JKT Msange - Tabora, JKT Ruvu - Pwani, JKT Mpwapwa   Dodoma, JKT Mafinga - Iringa, JKT Mlale - Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba -Tanga, JKT Makuyuni - Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, na JKT Mtabila - Kigoma, JKT Itaka - Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa - Rukwa, JKT Nachingwea - Lindi na JKT Kibiti- Pwani na Oljoro JKT- Arusha.

 

Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) waripoti katika kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

Aidha, kutokana na ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID-19) Nchini, Tahadhari za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo zitachukuliwa kipindi chote vijana watakapokuwa makambini.

 

JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo.

   1. Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia                       magotini, isiyo na zipu.

   2. T-shirt ya rangi ya kijani (Green Vest)

   3. Raba za michezo zenye rangi kijani au blue.

   4. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.

   5. Soksi ndefu za rangi nyeusi.

   6. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.

   7. Track suit ya rangi ya kijani au blue

   8. Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.

  

Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote waliochaguliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.

Kuona orodha kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa na maeneo ya makambi ya JKT waliyopangiwa bofya kwenye jina la kambi hapo chini.

 

 

 

 BOFYA JINA LA KIKOSI HAPO CHINI  KUANGALIA MAJINA JA VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA 2020 

 

 

 

 Tafadhali bonyeza jina la kikosi kutafuta jina lako

 BULOMBORA -KIGOMA  RWAMKOMA - MARA  KANEMBWA-KIGOMA
     
 MSANGE - TABORA  MPWAPWA - DODOMA  RUVU - PWANI
     
 MGAMBO - TANGA  MARAMBA - TANGA  MLALE - RUVUMA
     
 MAFINGA - IRINGA  MTABILA - KIGOMA  MAKUYUNI - ARUSHA
     
 ITAKA - SONGWE  LUWA - RUKWA  KIBITI - PWANI
     
 NACHINGWEA - LINDI  MILUNDIKWA - RUKWA  OLJORO - ARUSHA

 

 

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,

Makao Makuu ya JKT,

Tarehe 16 Julai 2020.

Uadilifu

JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa

Umoja na Mshikamano

Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.

Kujitolea

Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.

Uzalendo

Huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.

Nidhamu

Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.

Kupenda kazi

Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi