Jumatatu, 13 Julai 2020
Super User

Super User

MAJINA YA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA IDARA YA UHAMIAJI

                                                                                                                                                    

 

                                                             

                                                                 TAARIFA KWA UMMA

 

                          WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA IDARA YA UHAMIAJI.
 

 

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linautangazia Umma orodha ya majina ya vijana wa JKT Operesheni Kikwete

na Operesheni Magufuli waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Idara ya Uhamiaji.
 

Vijana hao wanatakiwa kuripoti katika Chuo cha Uongozi JKT kilichopo Kimbiji Jijini Dar es Salaam

kuanzia tarehe 14 Septemba 2019 hadi tarehe 15 Septemba 2019, tayari kwa kuanza mafunzo hayo.
 

Uteuzi huo unafuatia usaili uliofanywa na Idara ya Uhamiaji mwezi Agosti 2019 kwenye Kambi ya

Mgulani JKT jijini Dar es Salaam .
 

Kuona orodha kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa bofya_hapa na kuona aina ya vifaa

wanavyotakiwa kwenda navyo bofya_hapa.
 
 
 
 
                                                                                               Imetolewa na:

                                                                                               Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,

                                                                                               Makao Makuu ya JKT,

                                                                                               Tarehe 03 Septemba 2019. 

uhamiaji

                                                                                                                                    

 

 

                                                                                                                                         

TAARIFA KWA UMMA

WITO WA KUJIUNGA KATIKA USAILI WA NAFASI ZA KAZI IDARA YA UHAMIAJI.

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linatangaza wito wa kujiunga na usaili wa nafasi za kazi katika Idara ya Uhamiaji kwa wahitimu wa mafunzo ya JKT kundi la kujitolea operesheni Kikwete na Operesheni Magufuli waliopo katika makambi ya JKT na wale waliokwishamaliza mkataba na kurudi  majumbani kwao.

Vijana hao wanatakiwa kuripoti katika Kambi ya JKT Mgulani iliyopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki katika usaili huo utakaoanza tarehe 10 Agosti 2019 hadi tarehe 14 Agosti 2019 ukisimamiwa na maafisa kutoka Idara ya Uhamiaji.

Aidha, vijana watakaokuwa na sifa wanatakiwa kujitegemea kwa gharama za malazi, chakula na usafiri kwa muda wote watakaokuwa katika usaili.

Sifa ya kujiunga na usaili huo ni kama ifuatavyo:

 1. Awe raia wa Tanzania mwenye afya njema kimwili na kiakili.
 1. Awe hajawahi kushitakiwa na kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai nchini au nje ya nchi.
 2. Mwenye uwezo wa kuzungumza na kuandika lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha zaidi, mwenye uwezo wa kuandika, kuzungumza lugha nyinginezo za kimataifa watapewa kipaumbele kwanza.
 3. Mwenye umri wa kuanzia miaka 18 mpaka miaka 30.
 4. Awe tayari kuhudhuria na kuhitimu mafunzo ya awali ya askari wa uhamiaji kwa kipindi kisichozidi miezi tisa katika chuo chochote cha kijeshi.
 5. Mwenye shahada ya kwanza/ stashahada ya Juu kutoka chuo cha Elimu ya Juu au taasisi inayotambuliwa na Serikali, waombaji wenye shahada ya TEHAMA, Uhandisi mitambo, Umeme, Eletroniki na Mawasiliano ya Umma, Usanifu wa Majengo, Lugha za Kimataifa, Mass Communications/ Journalism, Project Management and Evaluations watapewa kipaumbele.

Vijana wenye sifa wanatakiwa kufika kwenye usaili wakiwa na vitu vifuatavyo:

 1. Cheti halisi na nakala moja ya cheti cha kuzaliwa mwombaji.
 2. Nakala ya vyeti vya kuhitimu elimu ya darasa la saba, Kidato cha nne, kidato cha sita na shahada ya juu kutoka chuo au taasisi yoyote inayotambuliwa na serikali. 
 1. Cheti halisi cha kuhitimu Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa na kalamu.

 

 

                                                                                                                                                       

 

Imetolewa na: 

                                                        Kurugenzi ya Habari na Uhusiano 

                            Makao Makuu ya JKT                                                 

Tarehe 03 Agosti 2019

 

 

 

 

MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA TATU 2019

 

 

TAARIFA KWA UMMA

           WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MUJIBU

WA SHERIA AWAMU YA TATU MWAKA 2019.

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza awamu ya tatu ya orodha ya majina ya vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2019, kutoka shule mbalimbali za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.

Sanjari na uchaguzi huo, JKT limewapangia vijana hao, makambi ya JKT watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 26 June 2019 hadi tarehe 05 Julai 2019.

Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho, (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti kambi ya JKT Ruvu iliyopo eneo la Mlandizi mkoani Pwani ambayo imejengewa miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

Mkuu wa JKT, anaendelea kuwakaribisha vijana wote waliochanguliwa ili waweze kuungana na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.

Orodha kamili ya majina ya vijana waliochanguliwa awamu ya tatu, maeneo ya makambi ya JKT waliyopangiwa na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz

 

KUONA MAJINA HAYO BOFYA HAPO CHINI

BULOMBORA-KIGOMA

RWAMKOMA-MARA

KANEMBWA-KIGOMA

MTABILA-KIGOMA

MPWAPWA-DODOMA

MARAMBA-TANGA

MAKUYUNI-ARUSHA

MAFINGA-IRINGA

MLALE-RUVUMA

NACHINGWEA-LINDI

ITAKA-SONGWE

LUA-RUKWA

MILUNDIKWA-RUKWA

 

Imetolewa na:

Kurugenzi wa Habari na Uhusiano

Makao Makuu ya JKT

Tarehe 25 Juni 2019

VIJANA MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA PILI 2019

 

 

 

 

 

                                                                                                                        

 

 

TAARIFA KWA UMMA

WITO WA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA KUJITOLEA.

 

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) anawatangazia Vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani nafasi za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea  kwa mwaka 2019.

 

Utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo unaratibiwa na ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambapo muombaji anaishi.

 

Zoezi la kuchagua vijana linaanza mwezi Juni 2019. Vijana watakaochaguliwa wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliopangiwa  mwezi Agosti 2019.

 

Aidha, kwa upande wa vijana wa Mujibu wa sheria, Jeshi la Kujenga Taifa limetoa orodha ya awamu ya pili ya majina ya vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita 2019 kwa ajili ya kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria.

 

Vijana hao wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliopangiwa kuanzia tarehe 11 Juni 2019 hadi tarehe 16 Juni 2019.

 

Orodha kamili ya majina ya vijana wa mujibu wa sheria waliochaguliwa awamu pili na makambi ya JKT waliopangiwa na aina ya vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go tz.

 

Mkuu wa JKT anawaalika vijana wote waliopata fursa hiyo kuja kujifunza Uzalendo, Ukakamavu, Stadi za kazi, na stadi za maisha zitakazowasaidia kujiajiri mara baada ya kumaliza mafunzo hayo.

 

Sifa za Muombaji ni kama ifuatavyo-:

1.  Awe raia wa Tanzania

2.  Umri

           a.  Kwa kijana wenye elimu ya darasa la saba umri ni kuanzia miaka 16 hadi 18.

           b.  Vijana wenye elimu ya kidato cha Nne umri usiwe zaidi ya miaka 20.

           c.  Vijana wenye elimu ya kidato cha sita umri usizidi miaka 22.

           d.  Vijana wenye elimu ya Stashahada umri usizidi miaka 25.

           e.  Wenye elimu ya Shahada umri usizidi mika 26.

           f.  Shahada ya uzamili umri usiwe zaidi ya miaka 30.

           g.  Vijana wenye elimu ya Shahada ya Uzamivu umri usizidi miaka 35.

3. Awe na afya njema,akili timamu na asiwe na alama yoyote ya mchoro mwilini (Tatto).

4. Mwenye tabia na nidhamu nzuri na hajapatikana na hatia Mahakamani na hajawahi kufungwa.

5. Kwa vijana waliomaliza elimu ya Sekondari kidato cha Nne awe waliomaliza 2016,2017,2018 na wenye ufaulu ufuatao.

            a. Wawe wamefaulu na wawe na alama(Points zisizopungua 32).

            b. Kidato cha sita wawe na ufaulu daraja la kwanza hadi daraja la Nne.

6. Awe na elimu ya msingi aliyehitimu darasa la saba.

      

7. Awe na cheti halisi cha kuzaliwa shule (Original Birth Certificate).

8. Awe na cheti halisi cha kumaliza shule (School Leaving).

9. Awe na cheti cha matokeo (Original Academic Certificate /Transcript.

10. Asiwe ametumikia Jeshi la Polisi,Magereza, Chuo cha Mafunzo au KMKM wala kuajiliwa na Idara nyingine Serikalini.

11. Asiwe amepitia JKT Operesheni za nyuma.

12. Asiwe amejiushisha na matumizi ya madawa ya kulevya bangi, na yanayofanana na hayo.

13. Kwa wale wenye Vipaji vya Michezo mbalimbali na Sanaa sifa za elimu nia sawa na zilizotajwa hapo juu.

 

JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo:-

1.  Bukta ya rangi ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni (lastic) iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini isiyo na zipu.

2.  Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.

3.  Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.

4.  Soksi ndefu za rangi ya nyeusi.

5.  Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.

6. Truck suit ya rangi ya kijani au blue.

7.  Flana ya kijani kibichi yenye kola ya duara isiyo na maandishi.( dark green Tshirt with round colar).

8. Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.

 

MAJINA YA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA KWA AWAMU YA PILI YANAPATIKANA KWENYE MAJINA YA MAKAMBI YA JKT YALIYOPO HAPO CHINI.

 

JKT BULOMBOLA

JKT ITAKA

JKT KANEMBWA

JKT LUWA

JKT MAFINGA

JKT MAKUTUPORA

JKT MAKUYUNI

JKT MARAMBA

JKT MGAMBO

JKT MILUNDIKWA

JKT MLALE

JKT MPWAPWA

JKT MSANGE

JKT MTABILA

JKT NACHINGWEA

JKT RUVU

JKT RWAMKOMA

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,

Makao Makuu ya JKT,

Tarehe 10 Juni 2019.

 

VIFAA AMBAVYO VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA 2019 WANATAKIWA KURIPOTI NAVYO MAKAMBINI

                                                                                                                                      

 

 

TAARIFA KWA UMMA

 

Vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria mwaka 2019 wanatakiwa kuripoti makambini na vifaa vifuatavyo:-

 1. Flana ya rangi ya kijani kibichi yenye kora ya duara (Dark Green T-shirt with round collar).
 2. Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
 3. Raba za michezo zenye rangi kijani au blue.
 4. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
 5. Soksi ndefu za rangi nyeusi.
 6. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
 7. Track suit ya rangi ya kijani au blue
 8. Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.

 

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,

Makao Makuu ya JKT,

Tarehe 24 Mei 2019.

Uadilifu

JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa

Umoja na Mshikamano

Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.

Kujitolea

Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.

Uzalendo

Huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.

Nidhamu

Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.

Kupenda kazi

Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi