Jumatatu, 13 Julai 2020
Super User

Super User

TAARIFA KWA UMMA

                                                                                                                                   

 

 

 

TAARIFA KWA UMMA

 

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Martin Busungu  leo amezindua magari manne ya kusambaza maji ya kiwanda cha Maji cha SUMAJKT yenye thamani ya Tsh milioni 310.

 

Sherehe ya uzinduzi huo, imefanyika Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa, Mlalakuwa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Wakuu wa Matawi na Wakurugezi wa Jeshi hilo.

 

Meja Jenerali Busungu amesema kuwa kupatikana kwa magari hayo kutapunguza changamoto kwenye soko iliyokuwa inaikabili kiwanda hicho haswa katika usambazaji wa maji kwenye jiji la Dar es Salaam na mikoa jirani.

 

Mapema akimkaribisha Mkuu wa JKT, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT, Kanali Ahmed Abbas amesema kuwa magari hayo siyo tuu yameongeza chachu ya usambazaji na uuzaji wa maji bali pia yatainua pato na kuendelea kujenga uwezo wa kiuchumi wa  kiwanda hicho.

 

Kiwanda cha SUMAJKT Bottling Plant Mgulani kilianza shughuli za uzalishaji mwezi Februari 2018 na kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli tarehe 17 Mei 2018 ikiwa ni kutekeleza kauli mbiu ya ujenzi wa Tanzania ya Viwanda.

 

 

 

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,

Makao Makuu ya JKT,

Tarehe 18 Desemba 2018.

Uadilifu

JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa

Umoja na Mshikamano

Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.

Kujitolea

Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.

Uzalendo

Huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.

Nidhamu

Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.

Kupenda kazi

Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi