
Super User
KUSITISHWA KWA MAFUNZO YA JKT KUNDI LA KUJITOLEA KWA MWAKA 2020/2021
TAARIFA KWA UMMA
KUSITISHWA KWA MAFUNZO YA JKT KUNDI LA KUJITOLEA KWA MWAKA 2020/2021
Jeshi la Kujenga Taifa linapenda Kuutaarifu Umma kuwa Mafunzo ya JKT kwa Kujitolea kwa mwaka 2020/2021 yaliyokuwa yaanze hivi karibuni katika makambi mbalimbali nchini, Mafunzo hayo yamesitishwa kwa muda mpaka hapo itakavyotangazwa.
Kutokana na Kusitishwa kwa mafunzo hayo, JKT linawataka Vijana wote ambao walichaguliwa na kuripoti makambini kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Kujitolea, Warejee majumbani kwao, na wale ambao walikuwa bado hawajaripoti wasiende kuripoti katika makambi waliyopangiwa mpaka hapo itakapotangazwa tena.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya JKT,
Tarehe 19 Januari 2021.
UGENI KUTOKA MISRI
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Charles Mbuge akimkabidhi zawadi Mwambata Jeshi wa Misri Nchini Brigedia Jenerali Khaled Mousbah baada ya kikao cha Mashirikiano baina ya Majeshi ya Nchi hizo mbili hususani JKT, kwenye nyanja za kilimo uvuvi na viwanda.
ZIARA KILIMANJARO
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Charles Mbuge (kushoto) akipokea pongezi kutoka kwa katinu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt Aloyce Nzuki baada ya SUMAJKT kuanza ujenzi wa bweni la wanafunzi wa chuo cha uhifadhi wa wanyamapori (MWEKA) Mkoani Kilimanjaro.
ZIARA CHITA
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Venance Mabeyo akiteta jambo baada ya uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi wa umwagiliaji unaotekelezwa na JKT katika Kikosi chake cha Chita Moani Morogoro.
.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Venance Mabeyo akiteta jambo baada ya uwekaji wa jiwe la Msingi kwenye mradi wa umwagiliaji unaotekelezwa na JKT katika Kikosi chake cha Chita Mkoani Morogoro.
.
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Charles Mbuge (kushoto) akipokea pongezi kutoka kwa katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt Aloyce Nzuki baada ya SUMAJKT kuanza ujenzi wa bweni la wanafunzi wa chuo cha uhifadhi wa wanyamapori (MWEKA) Mkoani Kilimanjaro.
.
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Charles Mbuge akimkabidhi zawadi Mwambata Jeshi wa Misri Nchini Brigedia Jenerali Khaled Mousbah baada ya kikao cha mashirikiano baina ya Majeshi ya nchi hizo mbili hususani JKT, kwenye nyanja za kilimo, uvuvi na viwanda.
.
Mkuu wa JKT na Mwenyekiti wa Kamati Kazi na Mipango (KKM), Meja Jenerali Charles Mbuge aongoza Wajumbe wa Kamati hiyo Septemba 3, 2020 kujionea maendeleo ya ujenzi wa Kiwanda cha Mabati JKT kilichopo Jijini Dodoma, ambacho kinatarajia kuanza kazi hivi karibuni.
.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe Dkt. Binilith Mahange amkabidhi Mkuu JKT, Meja Jenerali Charles Mbuge Shilingi Milioni Mbili kwa ajili ya ujenzi wa Msitiki Chamwino- Dodoma, zilizotolewa na Waziri wa TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo Septemba 2020.