Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa, akizungumza na washiriki wa semina ya uzinduzi wa programu maalumu ya kuwasaidia vijana wanaojiunga na kuhitimu mafunzo ya JKT kwa kujitolea katika ukumbi wa Mabatini Mgulani jijini Dar es Salaam Aprili 04 mwaka 2016.
- Brigedia Jenerali Henry Kamunde, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina iliyoandaliwa na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), katika Kambi ya JKT Mgulani, ikiwashirikisha maafisa na askari wa vikosi vya JKT Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, inayolenga kuwasaidia vijana wanaohitimu mafunzo ya JKT kwa kujitolea kujiajiri wenyewe.
- Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi Stadi (DVT) JKT, Kanali Chacha Wanyancha, akimkaribisha mgeni rasmi kufungua semina maalumu ya kuwawezesha vijana wa kujitolea wa JKT wanaohitimu mafunzo na kurudishwa nyumbani kujiajiri, iliyoandaliwa na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
- Washiriki wa semina ya programu maalumu ya kuwasaidia vijana wanaojiunga na JKT kwa kujitolea na kuhitimu, wakimsikiliza mgeni rasmi hayupo pichani, wakati wa ufunguzi uliofanyika ukumbi wa Mabati Kambi ya JKT Mgulani jijini Dar es Salaam.
10. Wakuu wa Vikosi kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Wakurugenzi wa Idara wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Brigedia Jenerali Henry Kamunde.